JESHI la polisi mkoani kagera linamshikilia Maiko Martine miaka ( 30 )mkazi wa mtaa wa Kyabitembe Kata Nshambya Tarafa Rwamishenye Manispaa ya Bukoba kwa tuhuma za kubaka watoto watatu wa darasa la tatu na la nne wa shule ya msingi Ithawa wenye umri kati ya miaka (10 )na (12 ).
Kamanda Maketi Msangi, leo amewaeleza waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo February 23 ,mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika msitu wa serikali wa Rwendimi uliopo Kijiji cha Ijuganyundo Manispaa ya Bukoba.
Alisema siku hiyo watoto hao walikuwa wameenda kuokota kuni kwenye msitu huo ndipo mtuhumiwa aliwavizia akawakamata na kuwatishia kuwakata na panga kama watapiga kelele na kisha kuwabaka .
Alisema baada ya kufanya kitendo hicho cha kikatili mtuhumiwa alikimbia kusikojulikana na kuogopa kukamatwa .
Alisema watoto hao walimtambua mtuhumiwa aliyewabaka kwa sura na alikamatwa Mei 24,mwaka huu majira ya saa moja na dakika hamsini jioni Kijiji cha Kyansonzi Kata ya Maruku halmashauri ya Bukoba.
CHANZO: TIMES MAJIRA
No comments:
Post a Comment