Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Damas Ndumbaro amesema wenye mamlaka na Katiba ya nchi ni wananchi wa pande zote za muungano na si suala la matakwa ya kikundi ama mtu mmoja.
Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Damas Ndumbaro
Aidha Waziri Ndumbaro aliupongeza mtandao kwa kuendelea kufanya kazi za utetezi wa haki za binadamu nchini kwa kipindi Cha miaka kumi na kwa ufanisi mkubwa,na kudai Serikali ipo nao bega kwa bega ili kuhakikisha inaboresha maisha ya Wananchi kwa lengo la kuwaletea Maendeleo wananchi.
" Miiaka 10 si mchezo inahitaji moyo wa kujitoa na ninashauri mtandao uendelee na kazi hiyo kwa moyo na serikali iko tayari kuwapa ushirikiano ili kuboresha maisha ya wananchi wetu",alisema Ndumbaro.
Kwa Upande wake mwakilishi wa Asasi za kiraia Bungeni, Mh Neema Lugangira akitoa salaam kwa wanamtandao na wadau aliishukuru Serikali kwa kuendelea kufanya kazi na asasi za kiraia na kutoa rai kwa wanamtandao kuweka kipaumbele kwa masuala ya lishe bora hasa kwa watoto si tu bali kubaki kutetea wananchi wakati hawapati lishe bora.
Wageni waalikwa wakiwa meza kuu wakiongozwa na Mratibu wa Mtandao Bwana Onesmo Olengulumwa kwenye mkutano wa kujadili uthibitisho wa mpango wa utekelezaji, mapendekezo ya UPR
No comments:
Post a Comment