JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limewaita vijna waliohitimu elimu ya Sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2022 kutoka shule zote za sekondari Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kuanzia tarehe 3 Juni 2022 na mwisho wa kuripoti ni tarehe 17 Juni 2022.
Akitoa taarifa kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema sanjari na wito huo Jeshi la Kujenga Taifa JKT limewapangia makambi watakyokwenda kuripoti na mwisho wa kuripoti ni Juni 17, 2022.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabena
Brigedia Jenerali Mabena amebainisha kuwa wahitimu wenye ulemavu unaoonekana kwa macho (Physical Disabilities) wanatakiwa kwenda kuripoti kambi ya 832KJ Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo inamiundombinu ya kuhudumia watu wenye jamii hiyo.
Pia, amefafanua kuwa orodha kamili ya majina ya vijana wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria, Makambi waliyopangiwa pamoja na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo ipo katika tovuti ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT ambayo ni www.jkt.go.tz.
Brigedia Jenerali Mabena amesema kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabena anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria ili waweze kuungana na wenzao kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, Stadi za Kazi, Stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa lao
No comments:
Post a Comment