Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Michael Mgombela (34) amefariki katika ajali ya gari aliyokuwa anaiendesha aina ya Toyota Hilux yenye namba za usajili T-840 DQF kugonga Kiberenge cha Treni mkoani Morogoro.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo Mei 23, 2022 katika makutano ya barabara na Reli eneo la Kilima hewa Manispaa ya Morogoro ambapo Kiberenge hicho chenye namba za usajili HDTC ni mali ya Shirika la Reli Tanzania.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa Polisi mkoani Morogoro Fortunatus Muslim amesema Kiberenge hicho kilikuwa kinatokea katika kituo cha Treni wilayani Kilosa kikielekea Morogoro mjini.
Kamanda amesema katika ajali hiyo mtu mwingine ambaye ni mwanamke ajulikanae kwa jina la Radhia Kassim (25) amejuruhiwa na anaendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo Kamanda Fortunatus Muslim amewataka watumiaji wa Barabara kuchukua tahadhali katika makutano ya Barabara na Reli ili kuepusha ajali ambazo zinaweza kuzuilika.
Chanzo:Millardayo
No comments:
Post a Comment