BASHUNGWA AWATAKA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA HOJA OR-TAMISEMI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 16 May 2022

BASHUNGWA AWATAKA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA HOJA OR-TAMISEMI

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amesema kwa kuwa sehemu kubwa ambayo ni asilimia 70 ya hoja zilizobainishwa na CAG, zipo ndani ya uwezo wa Halmashauri kuzifanyia kazi.


Hoja ambazo zimetokana na wataalam wa Halmashauri husika kutowajibika ipasavyo, hivyo Wakuu wa Mikoa wahakikishe wanaandaa mpango kazi wa utekelezaji hoja zote na taarifa iwasilishwe TAMISEMI kwa ajili ya ufuatliaji."


Akizungumza jijini hapa wakati akitoa taarifa ya ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2020/21 na hatua zilizochukuliwa kutekeleza maagizo ya CAG,
Pia, ameagiza kuwabainisha Watumishi wote ambao hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo, pamoja na wale ambao walijihusisha na vitendo vya ubadhirifu, na hivyo kusababisha hasara au hoja za ukaguzi zisizo za lazima.


"Watumishi hao wachukuliwe hatua stahiki za kinidhamu na kisheria na kuwasilisha taarifa za utekelezaji, Hatua hizo zitasaidia kuongeza umakini kwa Watumishi hao, na hivyo kupunguza hoja za ukaguzi zisizo za lazima katika miaka itakayofuata."


Bashungwa aliwataka Wakuu wa Mikoa washiriki Mikutano Maalum ya Mabaraza ya Madiwani, kujadili taarifa za CAG, na kutoa maelekezo yenye lengo la kuhakikisha kuwa hoja zote za ukaguzi zinafanyiwa kazi.


Aidha, amezitaka Ofisi za Wakuu wa Mikoa zihakikishe zinaratibu na kuweka mazingira mazuri ya kufanyika kwa uhakiki wa majibu ya hoja za ukaguzi kwa wakati, na kutoa taarifa kuhusu hoja zilizofungwa.


"Kama kutakuwa na hoja ambazo hazitafungwa, yatolewe maelezo ya sababu za hoja hizo kutofungwa na mkakati uliowekwa kuhakikisha zinafanyiwa kazi na kufungwa."


Bashungwa pia amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri wahakikishe wanawawezesha na kuwatumia Wakaguzi wa Ndani kikamilifu katika kutathimini ufanisi wa mifumo ya udhibiti wa ndani na kuchukua hatua stahiki.


" Pia Kamati za Ukaguzi ziwezeshwe kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi ikiwa ni pamoja na kujiridhisha kuwa zimeundwa kwa kuzingatia miongozo iliyopo na pia kuhakikisha kuwa zinajengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao."


Kuhusu mikopo kwa halmashauri, Bashungwa alisema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki na mwongozo wa utoaji na usimamizi wa fedha za mikopo ya Halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kudhibiti madai ya ubadhirifu.


"Mfumo huo unatarajiwa kuanza kutumika katika Halmashauri kuanzia Julai Mosi mwaka 2022 ili kuweka uwazi na uwajibikaji kwenye utoaji mikopo hiyo,"

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso