Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar linamshikilia Kheir Mkombe Abdallah (39) Mkazi wa Fueni Pangani wilaya ya Magharibi B kwa tuhuma za kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wake wa kike (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 11 mwanafunzi wa darasa la tano.
Akithibitisha mbele ya waandishi wa habari leo Jumamosi Mei 21, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi ACP. Abdallah Mussa Amesema Mtuhumiwa huyo alifanya kosa hilo mnamo Mei 10, 2022 majira ya saa Nne usiku huko Fuoni Pangawe na baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa alimbilia kusikojulikana.
Amesema mtuhumiwa amekamatwa mnamo Mei 20, 2022 majira ya Saa saba mchana katika Kijiji na Kata ya Likongowele Mkoani wa Lindi.
"Kwa kuwa Jeshi la Polisi lina mkono mrefu limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kutumia kitengo kinachoshughulikia Makosa ya kimtandao ( Cyber- crime) na kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi" amesema Kamanda Mussa
Aidha Kamanda Mussa ameongeza kuwa taratibu za kisheria zitakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
CHANZO: LANGO LA HABARI
No comments:
Post a Comment