Katika mwaka wa fedha 2021/22, Halmashauri zimepanga kukusanya Shilingi Bilioni 863.9 kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani.
Katika kipindi cha mwezi Julai, 2021 hadi Machi 2022, Halmashauri zimekusanya jumla ya Shilingi Bilioni 675.8, ambayo ni asilimia 78 ya makisio ya mwaka.
Makusanyo hayo ni sawa na asilimia 104 ya lengo la robo tatu ya mwaka. Itakumbukwa kwamba bajeti ya makusanyo ya mapato ya ndani, ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, iliongezeka kutoka Shilingi Bilioni 814.96 katika mwaka wa fedha 2020/21, hadi Shilingi Bilioni 863.9 katika mwaka wa fedha 2021/22.
Uchambuzi wa taarifa za mapato ya ndani ya Halmashauri, katika kipindi cha Julai, 2021 Machi 2022, umeonesha kuwepo kwa ongezeko la mapato halisi yaliyokusanywa kwa kiasi cha Shilingi bilioni 118.4, ikilinganishwa na kiasi kilichokusanywa katika kipindi kama hicho, cha Julai, 2021 - Machi 2022, sawa na ongezeko la asilimia 21.
Katika kipindi hiki, Julai 2021 – Machi 2022, zipo Halmashauri ambazo zimeongeza jitihada katika ukusanyaji wa mapato, ikilinganishwa na kipindi kama hiki cha mwaka wa fedha 2020/21.
Halmashauri hizo ni Halmashauri za Wilaya za Ngorongoro (asilimia 34), Mtama (asilimia 36), na Kishapu (asilimia 36), Halmashauri ya Mji Bariadi (asilimia 36), na Halmshauri ya Manispaa ya Lindi (asilimia 36). Katika kipindi hicho cha Julai, 2021 - Machi, 2022 Halmashauri hizo zilikuwa za mwisho.
Pia zipo baadhi ya Halmashauri ambazo katika kipindi cha Julai, 2021 – Machi 2022, zimeshuka katika ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ikilinganishwa na kipindi kama hiki cha Julai, 2020 – Machi 2021.
Katika kundi hili Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ambayo iliongoza kwa asilimia 117, imeshuka kwa asilimia 38, kutokana na makusanyo yaliyotokana na ushuru wa huduma katika migodi, ambayo hayakuwa yamewekwa kwenye Bajeti, na kuonekana wemekusanya fedha nyingi ikilinganishwa na Bajeti. Hivyo, nazielekeza Halmashauri ziweke mazingira mazuri, ili kuwa na vyanzo ambavyo ni endelevu na vinavyoakisi uhalisia.
No comments:
Post a Comment