Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Morogoro, Fortunatus Muslimu amesema mwanaume huyo ana umri wa miaka 29 ni mkulima, chanzo marehemu alipokea ujumbe unaosomeka ni fedha ametumiwa kimakosa hivyo anapaswa kuzirejesha.
Kamanda amesema tukio hilo limetokea Mei 10, 2022 majira ya saa kumi jioni, baada ya ujumbe huo marehemu alikwenda kukopa fedha hizo na kuzituma baadae alikwenda kwa wakala kutoa fedha hizo ili kwenda kulipa deni alikokopa lakini alivyofika kwa wakala aliambiwa ujumbe ule ulitumwa kwa makossa na hauna fedha yoyote.
“marehemu alijinyonga kwa kutumia Kamba ya katani kwenye mti wa mfenesi kutokana na kuhofia kudaiwa deni la laki nne”.
Hata hivyo kamanda Fortunatus Muslimu ametoa wito wa wananchi kuwa makini na simu zao pindi wanapopokea ujumbe kama huo wanapaswa kujiridhisha.
CHANZO:MILLARD AYO
No comments:
Post a Comment