AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI AKIVUA SAMAKI ENEO LA MGODI KISHAPU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 23 May 2022

AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI AKIVUA SAMAKI ENEO LA MGODI KISHAPU

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Mei 23,2022


Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Hamis Mayunga (27) mkazi wa Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ameuawa kwa kupigwa risasi na anayedaiwa kuwa Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Sam Security aitwaye Emmanuel Chacha katika eneo la Mgodi wa El – Hilal wilayani Kishapu.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Mei 23,2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Mei 20,2022 majira ya saa nne usiku katika eneo la mgodi wa El - Hilal.


“Hamis Mayunga (27) mkazi wa kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu aliuawa kwa kupigwa risasi na Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Sam Security yenye makao Makuu yake Mjini Shinyanga katika eneo la Mgodi wa El Hilal.


Huyu Hamisi Mayunga akiwa na wenzake wasiopungua 10 walikuwa wanavua samaki katika bwawa lililopo katika mgodi wa El – Hilal ndipo Mlinzi wa Kampuni ya Sam Security aitwaye Emmanuel Chacha akiwa na wenzake wanne waliondoka katika lindo lao walilopangiwa wakaenda katika bwawa hilo (ambalo siyo eneo lao la kazi, hawa hawafanyi doria) pakatokea kutoelewana ndipo akamfyatulia risasi kwa kututmia bunduki aina ya Shortgun ikampiga kwenye moyo upande wa kushoto na kusababisha kifo chake papo hapo”,ameeleza Kamanda Kyando.

CHANZO:MALUNDE 1 BLOG

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso