OPARESHENI TOKOMEZA PANYAROAD KUFANYIKA DAR, RC MAKALLA ATOA MAAGIZO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 2 May 2022

OPARESHENI TOKOMEZA PANYAROAD KUFANYIKA DAR, RC MAKALLA ATOA MAAGIZO



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ameagiza kufanyika oparesheni ya kuwasaka Panyaroad sambamba na kutolewa kwa taarifa za mafanikio ya oparesheni zitakazokuwa zinafanyika.


RC Makalla ametoa maagizo hayo wakati akitoa salamu za sikukuu za Eid El-ftir ambapo amesema misako itakayofanyika haitamuonea mtu na taarifa za oparesheni hizo zitolewe.


Amewahakikishia wananchi kusherekea sikukuu kwa amani na bila vurugu zozote kwenye maeneo yao kwani ulinzi unaimarishwa kila mahali ili kutokomeza wimbi hilo la uhalifu lilijitokeza.


Hata hivyo, Vijana wanaodhaniwa kuwa ni Panya road wamewakata mapanga watu 19 katika mtaaa wa Mtongani, Kata ya Kunduchi mkoani Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo Mei 2, 2022.


Tukio hilo limetokea masaa kadhaa tu tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, alipotoa onyo kwa vikundi hivyo kuachana na tabia hiyo, wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani iliyofanyika mkoani Dodoma.


Mmoja wa majeruhi hao amesema kwamba, vijana hao walikimbilia ndoo ya pesa, huku wakimuwahi kwa kumkata mikono yake ili akose namna ya kupambana nao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso