YANGA YATAMBA KUONESHA UKUBWA WAKE MECHI YAKE NA SIMBA 30 AAPRIL 2022 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 25 April 2022

YANGA YATAMBA KUONESHA UKUBWA WAKE MECHI YAKE NA SIMBA 30 AAPRIL 2022

Mashabiki na Wapenzi wa Yanga wametakiwa kutembea kifua Mbele na kujitokeza kwa wingi katika mchezo baina yake na watani wao, Simba kwani ni mechi ambayo wamedhamiria kuithibitishia Dunia kuwa ni timu kubwa Afrika Mashariki.


Akiongea na vyombo vya habari,Msemaji wa Yanga,Haji Manara,alibeza mbinu za hamasa zinazotumiwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba,Ahmed Ally kuwa ni dhaifu Kama haziwezi kulingana na zake.


Manara alidai Yanga haina inachoweza kujifunza kwa Simba kutokana na masuala yao kuendesha kizamani tofauti na Yanga ambayo inaendeshwa kiteknolojia zaidi na ndio maana inapata mafanikio kwa kasi.


Alijinasibu kuwa siku mahsusi ya kuthibitisha na  kuonesha ukubwa wa Yanga ni siku ya tarehe 30 dhidi ya Simba,ambapo  alijinasibu itakuwa ni siku ya furaha kwa wana Yanga hivyo wajitokeze kwa wingi.


".. sitegemei kuona Mwanayanga akibaki nyumbani siku hiyo. Sitotumia vispika vya kuuzia sumu ya Panya kufanya promotion,” Msemaji wa Yanga huku akimbeza Msemaji wa Simba.


Hata hivyo Manara alisema Yanga inakwenda kucheza mechi hiyo huku ikiwaheshimu watani zao,kutokana na kuwa  mabingwa watetezi, la pili wametoka kucheza mashindano ya Afrika.


Aidha alisema mbali na kucheza mashindano ya Afrika kwa bahati mbaya wametolewa, lakini licha ya kuwa ni mabingwa wanaotetea taji lao pia ni klabu kubwa kama ilivyo Yanga.


Alisema ni mechi ya Timu kubwa za Afrika Mashariki, na kamwe hawawezi kuwazungumza kwa kuwadharau wapinzani wao Kwa sababu wanaongoza kwa alama 13.


Alidai uongozi mzima pamoja na wachezaji pia benchi la ufundi wanajua ni mechi ambayo wanayanga wanahitaji ushindi,hivyo  lazima watacheze kwa nidhamu kubwa, maarifa makubwa,pasipo kuidharau Simba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso