Jeshi la polisi katika mikoa ya kipolisi ya Ilala, Temeke, Kinondoni, Pwani na Rufuji limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 632 walikamatwa, silaha/bunduki za moto 5, Pistol bandia 1 na risasi 53, Magari 9 Pikipiki 65 za wizi na mitambo ya kutengezeza gongo.
Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi operesheni hiyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro amesema hatua hiyo ni matunda ya makubaliano ya pamoja, kuhakikisha hali ya usalama inaimarika katika mikoa hiyo ya kipolisi sambamba na kupambana na makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha, na usafirishaji wa dawa za kulevya.
Amesema oparesheni hiyo ilifanikiwa kukamata madawa ya kulevya ya viwandani (Heroini kete 88 na Gramu 250) na bhangi; Gunia 31, Puli 520, Kete 5695 Misokoto 1726, Hekari 6 za shamba la Bhangi, kilo 46 za mbegu za Bhangi na Mirungi Kg 4.5, jino la Tembo, vyombo mbalimbali na vifaa vya kielektoniki vilivyotokana na matukio ya uvunjani nyumba pia vilipatikana.
Kuhusu makosa ya uhamiaji haramu, operesheni hiyo imefanikisha kukamatwa kwa Raia 45 wa Ethiopia na Somalia ambao walikabidhiwa Jeshi la Uhamiaji kwa mahojiano zaidi.
Jeshi la Polisi kwa kupitia Mikoa hiyo inaomba Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu, pia Jeshi linaahidi kuzitunza siri za watoa taarifa kwani malengo ya Mikoa hii ni kuendelea kuwa shwari
No comments:
Post a Comment