Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Festo Kiswaga ameiagiza kampuni inayohusika na ujenzi wa barabara ya Kahama-Ushetu kuhakikisha wanaondoa mawe yaliyopo barabarani ili kuepusha ajali barabarani.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndugu Festo Kiswaga akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama
Na Taikile Turo/Sada Salum - Huheso Blog
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa Bukondamoyo kufuatia Wananchi hao kufunga barabara baada ya ajali iliyotokea barabarani hapo kwa mtoto kugongwa na gari.
Amesema kitendo cha Wananchi hao kufunga barabara ni hatari kwani inaweza kusababisha madhara makubwa kwa wananchi wengine kwani barabara hiyo imekuwa ikitumika muda wote.
Aidha, mkuu wa Wilaya ameliagiza jeshi la polisi kumkamata
mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Bukondamoyo kwa kosa la
kuhamasisha wananchi kufunga barabara kutokana na ajali hiyo huku akisema asikamatwe mwananchi yoyote.
“Jeshi la polisi huyu mwenyekiti mchukueni tukaelewane nae vizuri kwa sababu amejichukulia sharia na kuhamasisha kufunga barabara hilo ni kosa sawa na la mauaji kwa sababu unaweza kufunga barabara akifika hapa mama mjamzito anakwenda hospitali hawezi kupita kisa mmefunga barabara”.
Kiswaga amesema wazazi na walezi wanalo jukumu la kuhakikisha watoto wao wanakuwa salama na kuhakikisha wanawasaidia kuvuka barabara huku akilitaka Jeshi la polisi kuhakikisha linatoa elimu ya usalama barabarani kwa wananchi muda wote wanapopata nafasi.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya, Festo Kiswaga amemuagiza Mkrugenzi wa kampuni ya ujenzi wa barabara hiyo Emmanuel Magema kufika leo na kuongeza kuwa wakandarasi wanaotumia muda mrefu kukamilisha miradi ya maendeleo hawatakiwi.
No comments:
Post a Comment