Baadhi ya vijana nchini Zimbabwe wameripotiwa kuchukua kemikali zinazotumika kwenye taulo za kike (Pedi) na nepi (Diapers) na kuzitumia kama kilevi cha bei nafuu.
Vijana hao wamedai kwamba huchukua kemikali inayojulikana kama sodium polyacrylate kutoka kwenye bidhaa hizo na kuzichemsha na huunda utando wa kijivu na kuunywa mchanganyiko huo.
Kemikali hiyo nayojulikana kama sodium polyacrylate ndiyo inayotumika kunyonya damu ya hedhi kwenye taulo za kike 'pedi' na mkojo kwenye nepi za watoto 'diapers'.
CHANZO: EATV NEWS
No comments:
Post a Comment