Watalaamu kutoka Shirikisho la soka barani Afrika CAF wanatarajia kutua nchini kesho kwaajili ya kufunga vifaa vya teknolojia ya VAR kwa ajili ya mchezo wa robo fainali baina ya Simba dhidi ya Orlando pirates utaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, ,jijini Dar es salaam.
Meneja wa uwanja wa Mkapa , Nsajigwa Godwin amesema hayo huku akithibitisha maandalizi muhimu kuwa tayari kwa ajili ya kufungwa kwa teknolojia hiyo kuelekea mchezo huo wa jumapili ambapo utatazwa na mashabiki elfu sitini.
''Ni faraja kwetu VAR kuja nchini na hii inatupa somo ya namna gani ya kufunga mfumo huu nakujua unavyofanya kazi ili ule mchakato wa serikali katika kununua VAR ukija tunakuwa tunajua vitu vichache katika teknolojia hiyo'' amesema Nsajigwa.
Pia meneja huyo ametoa rai kwa mashabiki kuwa wazalendo pindi wanapokwenda uwanjani hususani kutunza miundombinu ya uwanja huku hatua kali zaidi zitachukuliwa kwa wale wenye tabia ya kuvunja au kuharibu miundombinu ya uwanja
No comments:
Post a Comment