Wizara ya Afya imepata kibali cha ajira 1650 za Wataalamu wa kada mbalimbali za Afya ambao wataajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi ambavyo vipo chini ya uendeshaji wa moja kwa moja wa Wizara ya Afya.
Kibali cha nafasi hizo za ajira 1650 kutoka Ofisi ya Rais – UTUMISHI kinatoa fursa kwa wataalamu wa kada mbalimbali katika vituo vya kutoa huduma chini ya uendeshaji wa moja kwa moja kwa Wizara ya Afya.
Muda wa kutuma maombi haya ni ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili (kuanzia tarehe 16/04/2022). Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Wizara ya Afya unaopatikana kupitia tovuti: ajira.moh.go.tz.
Muombaji atakayeomba kupitia ya Wizara ya Afya, ASIOMBE kwa nafasi hiyo hiyo kwa upande wa OR-TAMISEMI.
No comments:
Post a Comment