RAMADHANI : KUFUNGA NI NINI? - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 12 April 2022

RAMADHANI : KUFUNGA NI NINI?




Kufunga ni nini?

Kufunga ni kujiepusha na chakula, vinywaji na kuwa na mahusiano na mwenzi wako kwa makusudi kuanzia alfajiri (wakati wa Alfajiri inapoanza na wakati wa Suhur unaisha) hadi kuzama kwa jua (wakati Magharibi inapoanza).

Je, nitaanzaje kufunga?

Saumu huanza mara tu unapoweka nia ya kufunga na kwa hivyo unaepuka kufanya chochote kinachofungua.

Makusudio hayahitaji kusemwa kwa maneno, wala hakuna Dua ya kuanzisha saumu.

Kwa mfungo wowote ule kando na Saumu za Qada (mfungo uliokosa ambao hufungwa tena baadaye), una muda wote hadi adhuhuri (wakati wa Zawal/Zuhr) kuamua kama unataka kufunga au la.

Maana yake ni kwamba ikiwa mtu atajisikia vibaya na akaamua kutofunga wakati wa Suhur, lakini hakula chochote mpaka kidogo kabla ya Adhuhuri, na akajisikia vizuri na akaamua kufunga, basi funga yao itahesabiwa maadamu sio Qada.

Ikiwa ni Saumu ya Qada, nia lazima itolewe kabla ya Saumu kuanza Alfajiri.

Nani anapaswa kufunga?

Yeyote anayekidhi vigezo vifuatavyo ni lazima afunge:

Aliyebalehe kufikia wastani wa umri wa balehe wa miaka kumi na nne na nusu katika kalenda ya Gregorian)

Mwenye akili timamu - mtu yeyote anayesumbuliwa na ugonjwa wa akili ambao ama huwafanya wasijue kufunga, au wasiweze kuelewa wazo la kufunga (kama vile wale wanaosumbuliwa na Down Syndrome) hawatalazimika kufunga.

Ikiwa si mgonjwa na mwenye magonjwa sugu ambayo huzuia kufunga, kama vile kisukari kali, au hata udhaifu kutokana na uzee.

Msafiri ambaye haendi safari ya zaidi ya maili arobaini na nane.

Kufunga hakutamdhuru mtu au mtoto wake (ikiwa mwanamke ni mjamzito au ananyonyesha).

Je, vipi ikiwa mtu anaruhusiwa kutofunga?

Ikiwa mtu kwa kweli anahisi kuwa hapaswi kufunga kwa sababu mbili za mwisho, anapaswa kuthibitishwa na daktari, daktari wa Kiislamu ambaye anaelewa umuhimu wa Kiislamu wa kufunga pamoja na kuangalia afya yako, badala ya kuangalia tu madhara ambayo inaweza kuwa nayo.

Ingawa afya ni muhimu sana kwa vile miili yetu ni amana kutoka kwa Allah Taala, tunapaswa kukubali tu ikiwa tunahitaji - si kwa sababu tu tunaweza kuwa wadhambi vinginevyo, lakini kwa sababu tunapaswa kuhisi kwamba tunakosa malipo na faida nyingi za kufunga.

Ama wasafiri, ingawa wameondolewa, kama wanaweza, wao pia wanapaswa kufunga ikiwa hali si ngumu.

Katika zama za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kusafiri kulihitaji kuvuka majangwa kwenye joto linalowaka kwa muda wa wiki na hatari ya upungufu wa maji mwilini.

Kwa sababu safari imekuwa rahisi, tunapaswa kujaribu kufunga kama tunaweza.

Mwishowe, ingawa watoto ambao sio Baligh wamesamehewa, wao pia wanapaswa kuhimizwa kufunga kutoka kwa umri mdogo ikiwa wako tayari na haiathiri afya au masomo yao.

Mazingira ambayo kila mtu anakula Suhur na Iftar yake pamoja, anaswali Tarawih msikitini pamoja (au nyumbani kwa wasichana na mama zao), pamoja na mawaidha ya mara kwa mara ya malipo ya Allah Taala, yatajenga hisia ya kudumu ya kukumbukwa na watoto ambayo huwafanya wasiishie na Ramadhani tu wakiwa wakubwa, bali waipende pia.

Iwapo mtu hawezi kufunga kwa dhati, atatakiwa kutoa Fidya, ambayo ni kutoa kiasi kilichotolewa kwa ajili ya Sadaqatu'l Fitr kwa kila siku ambayo hawezi kufunga.

CHANZO BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso