Na, Paschal Malulu-Manyara
Jeshi la Polisi mkoani Manyara limethibitisha mwanaume mmoja ajulikanae kwa jina la Simon Zakalia (58) kufanya ubakaji wa watoto watatu wilayani Hanang mkoani humo.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Manyara, Limited Mhongole amethibitisha akisema mtuhumiwa huyo alitenda ukatili huo mwaka uliopita 2021 kwa nyakati tofauti ambapo tukio la kwanza mtuhumiwa alimbaka mwanafunzi akiwa shambani.
Tukio la pili ni mwanaume huyo alimbaka
mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi ambapo
alimlazimisha kufanya kitendo hicho.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo tayari
amekamatwa na yupo mahabusu.
Msikilize Kamand Limited Mhongolo Kutoka Manyara
No comments:
Post a Comment