Na Taikile Turo
Mahakama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imemuhukumu kifungo cha maisha jela Baraka Andrea (26) mwalimu wa Tuition baada ya kukutwa na hatia ya kulawiti watoto watatu wa shule ya Msingi Majengo wenye umri chini ya miaka 10.
Akisoma hukumu hiyo leo April 25, 2022 mbele ya Mahakama hiyo Hakimu Donasian Agustino amesema Mahakama inamhukumu
mshtakiwa kwa mujibu wa kifungu namba 154(a) na 2 sheria kanuni ya adhabu.
Amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani umejitosheleza bila kuacha shaka hivyo Mahakama inamtia hatiani mshitakiwa huyo kwa kosa hilo la ulawiti.
Kabla ya Hakimu kusoma hukumu hiyo, mwendesha mashitaka Satuninus Kamala aliiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Kwa upande wake
mshitakiwa Baraka Andrea ameomba kupunguziwa adhabu kwani ana familia
inayomtegemea.
Hata hivyo mbali na
mshtakiwa kuomba kupunguziwa adhabu tayrai mshtakiwa alikuwa anatumikia kifungo
cha maisha gerezani kwa kesi nyingine ya kulawiti hivyo mahakama imetupilia
mbali ombi hilo.
Chanzo:Mahakama
Aiseee Mungu tusaidie maana tulipo sasa tutakosa kuaminiana kabsa hadi mwalim nawaza tu vipi kwa wanafunzi wake☹️
ReplyDelete