Jeshi la polisi mkoani Tabora linamshikilia mtu mmoja aliyefamika kwa jina la Ibrahim Evalist mwenye umri wa miaka 33 kwa tuhuma za mauaji ya mwalimu Hamza Mustapher mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa kata ya mkolye wilaya ya sikonge.
Na Amisa Mussa - Huheso Blog Tabora
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao
Akitoa taarifa Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea april 20 mwaka huu majira ya saa nne usiku katika kijiji na kata ya mkolye wilaya ya Sikonge ambapo chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi na mbinu iliyotumika ni kumvizia njiani mwalimu Hamza akiwa anatokea msikitini na kutekeleza mauaji hayo.
Pia Kamanda Abwao amesema mafaniko yote haya ya kuwabaini waharifu na uharifu yanatokana na kushirikiana na wananchi na kutoa wito kwa jamii ya mkoa wa Tabora kuendelea kuliamini jeshi la polisi kwa kutoa taarifa hizo za siri zitakazo saidia kukomesha vitendo vya uharifu mkoani hapa.
No comments:
Post a Comment