MPIGA DEBE AFARIKI KWA KUKANYAGWA NA TAIRI ZA GARI - NJOMBE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 23 April 2022

MPIGA DEBE AFARIKI KWA KUKANYAGWA NA TAIRI ZA GARI - NJOMBE

Mpiga debe mmoja wa eneo la Makambako Mkoani Njombe amefariki dunia kwa kukanyagwa na tairi za gari katika kichwa chake kutokana na kuanguka wakati akifukuzia basi linalofanya safari zake kutoka Mbeya kwenda mkoani Mwanza kwa lengo la kupata posho yake ya kupakia abiria.


RPC wa Njombe Hamis Issah amesema "Mpiga debe alikuwa amefuata fedha yake kwa ajili ya abiria aliokuwa amewapakia na kwa bahati mbaya ule malango wakati unajifunga alisukumwa na akadondokea kwenye uvungu na tairi za nyuma za gari ambazo zilimpitia”

RPC Issah ametoa wito kwa Wafanyakazi wa maeneo ya stendi kuwa makini na kuangalia usalama wao wakati wa kufanya kazi zao.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso