Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Stide Joackim mwenye umri wa miaka 34 mkazi wa kijiji cha Kyaka kata ya Kyaka wilaya ya Missenyi, kwa tuhuma za kumbaka binti mwenye umri wa miaka 16, mwanafunzi wa shule moja ya sekondari ambayo jina lake limehifadhiwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kagera ACP Maketi Msangi amesema kuwa, tukio hilo lilitendwa Aprili 18 mwaka huu katika kijiji cha Kyaka kata Kyaka, na kwamba mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni Aprili 20 mwaka huu saa 8:30 mchana, akiwa katika kijiji Bulfani kilichoko katika kata hiyo.
Aidha katika tukio jingine kaimu kamanda huyo amesema kuwa wamekamata maboksi 66 yenye vifaa vinavyotumika kusafirisha umeme kwenye laini kubwa ya umeme ya mkondo wa Kilovots 33, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18, katika msako maalumu uliofanyika kati ya Aprili 18 hadi 20 mwaka huu, na kwamba jitihada za kuwakamata watuhumiwa zinaendelea.
No comments:
Post a Comment