MANARA AWANANGA SIMBA BAADA YA MCHEZO WAO AFRIKA KUSINI. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 25 April 2022

MANARA AWANANGA SIMBA BAADA YA MCHEZO WAO AFRIKA KUSINI.


Na Ally Lityawi 

Siku moja baada ya Simba Kushindwa kufuzu hatua ya nusu Fainali ya michuano ya Shirikisho Barani Afrika,Mabingwa wa Kihistoria nchini,Yanga wameitisha Mkutano na waandishi wa Habari huku wakitupa kombora kwa watani zao wa jadi.


Wakitoa wito kwa vyombo vya habari kupitia ukurasa wa mtandao wa Kijamii wa Msemaji wao,Haji Manara,alisema lengo ni kuelezea wamejipanga kufanya nini wiki hii kuelekea pambano lao na Simba.

Katika andiko lake ambalo limetamalaki  utani huku akionesha dhahiri kumnanga Ahmed Ally,ambaye ametokea kuwa maarufu kwa wanazi wa Simba kiasi cha kufuta alama za Manara alizoacha Simba.

Haji aliandika kuwataka watani zao Simba kupitia kitengo Chao Cha  hamasa na promotion za football na michezo Kwa ujumla waketi na kumfuatilia ili kuchukua Elimu kwake juu ya suala hilo.

Aliwasihi kitengo Cha habari Cha Simba wawe pembeni ya Tv zao kujifunza namna ya kuadress umma na namna sahihi ya kuufanyia marketing mpira bila kutumia nguvu na kutoka mijasho. 

"Wanahabari Njoooni Saa Sita Mchana wa leo ili mkaujuze Umma nini tumekusudia kufanya wiki hii",alisema Manara.

Manara alijinasibu kwa kusema,"Don’t forget, Promo za Soka huwa hatutumii Vispika vya Wauza Dawa za Mende na Sumu za Panya, vile tuwaachie wao na wanaonunua Dola chakavu."

Aidha duru za Michezo zinabainisha kuwa Yanga wana lengo la kuanza shamrashamra za Ubingwa mapema,kutokana na uhakika wa kuifunga Simba katika mchezo wa April 30,Mwaka huu.

Duru hizo zilitanabaisha  kutokana na kuwa na kikosi Cha ushindi ambacho kwa Ligi ya ndani hakikuwa na mshindani zaidi ya Azam,huku wakijinasibu kuiandalia kipigo kikali Simba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso