AMUUA BABA YAKE KWA TUHUMA YA KUMKUTA ANAFANYA MAPENZI NA MKE WAKE SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 27 April 2022

AMUUA BABA YAKE KWA TUHUMA YA KUMKUTA ANAFANYA MAPENZI NA MKE WAKE SHINYANGA






Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kumuua baba yake mzazi Shija Robert (55), baada ya kumkuta amelala kitanda kimoja na mke wake.

Tukio hilo limetokea jana usiku katika mtaa wa Mwasele Mihogoni kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga chanzo cha tukio hilo kimetajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi baada ya marehemu kukutwa akiwa amelala kitanda kimoja na mke wa mtuhumiwa ambapo alimpiga na kipande cha kuni sehemu mbalimbali za mwili wake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa mtaa wa Mwasele Mihogoni bwana Richard Baluhi ameeleza namna alivyopokea taarifa za tukio hilo ambapo amesema mtuhumiwa huyo alienda na mke wake kumtembelea baba yake na kwamba tukio hilo lilotokea baada ya watu hao kutumia kilevi cha pombe.

“Mimi nilipigiwa simu nikaenda kwenye tukio nikaambia huyu marehemu ameuawa na kijana wake mkubwa wa kwanza kumzaa alimtembelea baba yake yeye anaishi ndala alikuwa na siku nne hapo kwa baba yake jana walitoka kwenda kutembea walipofika wakavyo pombe wakarudi nyumbani wamelewa ilipofika saa nne na nusu usiku kila mmoja akaenda kulala baada ya muda mfupi huyu mtuhumiwa alitoka nje kwenda chooni kujisaidia haja ndogo”

“Alipokuja kurudi huyo baba mtu alishaigia kwa mke wake na huyo mtuhumiwa na kwa sanbabu hiyo nyumba haina taa basi huyo kijana alikuwa na tochi alipomulika akamuona baba yake amelala kidanda kimoja na mke wake basi wakaanza kupigana humo ndani na badae wakatoana nje huyo kijana alichukua kipande cha kuni ndiyo basi akaanza mashambulizi akambiga mpaka kufa”. ameeleza mwenyekiti Baluhi

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema tayari jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa huyo huku likiendela kufanya uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso