Na Sada Salum:
Zoezi la utoaji chanjo ya Polio kwa wilaya ya kahama linatalajia kuanza mnamo April 28 na kukamilika May mosi mwaka huu katika maeneo yote ya wilaya ya kahama.
Akizungumza na wandishi wa habari ofini kwakwe mkuu wa wilaya ya kahama Festo Kiswaga amesema watoto kuanzia miaka sifuri hadi miaka mitano wanatakiwa kupata chanjo hiyo ya Polio ambayo itachukua muda wa siku nne kwa wilaya ya Kahama.
Pia Kiswaga amesema kwa wilaya ya kahama wanatarajia kuchanja watoto takribani laki moja na Elfu sabini katika halimashauli zote za wilaya ya Kahama ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Halmashauri ya wilaya ya Ushetu pamoja na Msalala.
Aidha mpaka sasa Tanzania kwa ujumla takwimu zinaonyesha hakuna mgonjwa yoyote wa Polio huku lengo likiwa ni kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa huo hatari.
Hata hivyo serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kiasi cha fedha takribani milioni mia tano na elfu hamsini kwa kila hospitali kwa ajili ya chanjo na vifaa tiba.
No comments:
Post a Comment