Watanzania wawakilishi, Simba kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho safari yao imefika kikomo leo nchini Afrika Kusini baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalty 4-3.
Mchezo ulikuwa mzito hasa kipindi cha kwanza,
Simba walipiga mpira mwingi kwa kujilinda huku viungo wakishindwa kutengeneza
nafasi kwa washambuliaji wao.
Idadi ilikuwa ni 1-1 na kuwafanya Simba waweze
kwenda kuamua mchezo kwa mikwaju ya penalti hapo ndipo ugumu unaanzia kutokana
na historia ya samba msimu huu hasa katika upigaji wa penati jambo ambalo samba
msimu huu kwenye upigaji wa penaji umekuwa mgumu kwao.
Simba ilikosa penati mbili kupitia kwa Jonas
Mkude na Henock Inonga huku Aishi Manula akiweza kuokoa penalti moja na ile ya
mwisho iliyopigwa na kipa wa Orlando ilizima ndoto za samba za kutinga nusu
fainali msimu huu na kuyaaga mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment