Kila Ramadhani huchukua siku 10 hadi 11, kwani miezi ya Hijri ni siku chache kuliko kalenda ya kawaida, ambayo ina maana kwamba kila mwaka Ramadhani inakaribia Januari.
Kwa mujibu wa mtaalamu wa Nyota Khalid al-Zaqaq, tofauti ya siku za hesabu hizo mbili ina maana kwamba kila baada ya miaka thelathini tunafunga mara mbili kwa mwaka. Mara ya mwisho hii ilifanyika mnamo 1997.
Unapotazama kalenda ya Saudi Arabia 2030 unaona kwamba Ramadhani ya kwanza itaanza Januari 6, huku Eid ikiangukia tarehe 5 Februari. Ramadhani ya pili inaangukia tarehe 26 Disemba mwaka huo huo.
Kutokana na hesabu hizo za wataalamu wa Nyota Waislamu watafunga kwa takriban siku 36, kukamilisha Ramadhani 1451H na Ramadhani 1452H kwa siku sita.
Mwaka wa Hijri una siku 354 au 355, wakati kalenda ya kawaida ina siku 365.
Wakati wa Ramadhani, nchi ambazo Waislamu hufunga saa nyingi zaidi ni Iceland, Uingereza, Ufaransa, Ureno na Poland. Wanafunga kwa zaidi ya masaa 16.
Nchi zenye saa fupi za kufunga ni New Zealand, Afrika Kusini, Paraguay na Uruguay zenye saa 11 hadi 12 za mfungo.
CHANZO BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment