Wakazi wa Kata ya Ulowa wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameingiwa na hofu dhidi ya matetemeko yanayojitokeza mara kwa mara hali ambayo imetajwa kuathiri nyumba zao.
Wananchi hao wameiomba serikali kupeleka wataalamu wa miamba ili kufanya utafiti wa tatizo hilo.
Baadhi ya nyumba za wakazi wa Kata hiyo zimeonekana
kuwa nya nyufa ambazo wanadai kuwa ni kishindo cha matetemeko ambayo yanatokea
mara kwa mara katika Kata ya Ulowa.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga
akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kahama ametembelea kujionea
baadhi ya athari zilizoanza kujitokeza dhidi ya tetemekeko hilona kuzungumza na
baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo.
Mkuu wa Wilaya, Festo Kiswaga amesema
kutokana na hofu ya wananchi pamoja na madai yao kuwa kumekuwa kunatokea na
matetemeko ameahidi kuleta wataalum kwa ajili ya kupima na kuona ni kitu gani
ambacho kinasababisha kuwa na tetemeko.
Kiswaga amewataka wananchi kutokuwa na
hofu kwani tayari jambo hilo linafuatiliwa na litatolewa ufafanuzi.
Nae mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji
Wilaya ya Kahama, Hanafi Mkilindi amesema tetemeko hilo halijaleta athari kwa
binadamu licha ya nyumba kuwa na nyufa ambazo zimetokea baada ya vishindo vinavyodaiwa
kuwa ni tetemeko.
No comments:
Post a Comment