ABDI BANDA
Jumapili ijayo Simba inaingia uwanja wa Benjamini Mkapa kupeperusha bendera ya nchi,katika mchezo wa Robo Fainali wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika baina yake na timu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Wakati wa uelekeo wa mchezo huo,zimeibuka tuhuma dhidi ya Simba kutoka kwa mchezaji wa Mtibwa Sugar na ambaye aliwahi kuichezea Simba kuwa timu yake hiyo ya zamani inanunua mechi za nyumbani katika michuano hiyo.
Banda katika madai take,Simba si nzuri kiasi Cha kufikia hatua hiyo na kumuomba Senzo Masingisa aipokee Orlando Pirates ili kuinusuru na mchezo mchafu wa Simba.
Huyo Ni Abdi Banda mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania aliyewahi kucheza soka la Kimataifa nchini Afrika Kusini,akitoa maneno yadiyo na afya na soka la nchini mwetu na TFF ambao Ni mzazi wa Soka letu ipo kimya.Je haioni madhara ya kauli hiyo?
Ilitarajiwa TFF ingeanza kumchukulia hatua za kinidhamu hasa kwakuwa Ni mchezaji anayecheza Ligi inayoisimamia kwa kumuita na kumuomba athibitishe kauli yake.
Lakini TFF wapo kimya kivipi ? Kwanini wawaachie jukumu hilo Simba pekee Yao?Kwani inayochafuliwa si Simba pekee? Bali Ni Nchi nao ndio wasimamizi wa Soka letu na itambulike hiyo Ni michuano ya Kimataifa ambapo wenyeji wa michuano hiyo Ni TFF.
Sasa Kama Simba wananunua mechi itakuwa kwa msaada wa TFF,ambayo inahusika na kuwapokea Watendaji katika mechi wanazocheza nyumbani wakiwemo wa waamuzi wa mchezo.
Hivyo kuchafuliwa kwa Simba katika michuano hiyo,TFF nayo inapakwa matope, vipi inakaa kimya na kuichia Simba pekee ambayo hakuna ubishi kuwa inalitangaza Soka la Tanzania Kimataifa kwa ngazi ya Vilabu.
Angalia wakati wa droo ya kupanga hatua za Michezo ya Robo Fainali,Kocha wa Al Masry ya Misri,Ahmed Shanded, alisema alipenda kukutana na Simba kwakuwa ndio timu inayoonesha ushindani.
Pia Kocha wa ASEC Mimosas,Julien Chevalier,naye alidai kundi lililokuwa timu yake ikijumuisha Simba ndio lilikuwa kundi la kifo na kulitabiria kutwaa Kombe hilo huku akiipa Simba asilimia 60 kutwaa Kombe Hilo.
Unapoitaja Al Ahly ama Zamalek umegusa soka la nchini Misri,sidhani kama Shirikisho la soka la nchi hiyo lingekaa kimya pindi ingetokea mchezaji mzalendo kutoa kashfa kwa timu hizo kama alivyofanya Banda.
Lakini TFF suala la kashfa ya kuchafuliwa Simba katika michuano hiyo ipo kimya,bali Simba imeamua kulishughulikia. Basi na ishughulikie katika misingi isiyoathiri soka letu.
Kwani ikikurupuka kwenda Mahakamani Basi soka la Tanzania kitaingia katika mgogoro na kufungiwa kushiriki michuano ya Kimataifa.Chanzo kitakuwa Banda.Hivyo Usalama wa jambo hili ni TFF kulibeba.
Banda Ni vyema aitwe kutoa uthibitisho wa mafanikio ya Simba Kimataifa yanatokana na rushwa,pengine Ana ushahidi kwa Hilo na atasaidia Vilabu vyetu kuondokana na Michezo michafu itakayokuja athiri Taifa pindi ikibainika na vyombo vinavyosimamia soka Kimataifa.
Alichoandika Banda kimezagaa duniani kote kwani kipo katika mtandao wa Kijamii,Ni dosari na kashfa kubwa kwa soka la Tanzania.
Ni vyema kujiuliza Banda aliondoka Simba,ikiwa na Hali mbaya haijaanza hata kushiriki michuano ya Kimataifa,Ni vipi Leo kadiriki kutoa kauli hiyo,huo mchezo mchafu wanaofanya kaubaini vipi ilhali si mwanafamilia wa Simba?
Je andiko lake lina maslahi gani na Orlando Pirates.Uzalendo wake kwa Taifa hili upo wapi na kwanini amtaje Senzo? Na kwanini Simba pekee wadai kulishughulikia kashfaa hiyo huku TFF ikiwa haina mpango wa kuchukua hatua?Hapa Kuna ukakasi.
Kama Banda akidai si yeye aliyeandika hivyo achukue hatua za kisheria kulinda hadhi yake ndipo Simba waendelee kuchukua hatua.Pindi ikidhihiri hivyo kwa Banda kuwa mkweli ama kutumika vibaya, na hata kuingiliwa akaunti yake,Basi Soka la Tanzania litakuwa limeingiwa na kirusi kibaya.
No comments:
Post a Comment