Mtoto mwenye umri wa miaka mitano (5) amenusurika kujeruhiwa na fisi majira alipokua eneo la shule ya msingi Mwabalange Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Tukio hilo limetokea leo Ijumaa April 22, 2022 majira ya saa nne Asubuhi mara baada ya mtoto huyo kuachana na baba yake aliyemsindikiza shuleni hapo.
Inaelezwa kuwa baba wa mtoto alimuona fisi akimvizia mwanae na kupiga kelele kuwaita wananchi wengine ambao walimkimbiza fisi huyo hadi kwenye pango na kupambana nae hadi kumuua.
Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange amesema kupatikana kwa fisi huyo ni matokeo ya operesheni za kuwasaka fisi kwenye mapango ya mjini Bariadi operesheni ambayo mbali na kufanywa mapangoni katika kata zote za mji wa Bariadi zimeendelea na operesheni hiyo hali iliyofanya fisi wakimbilie maeneo ya nje ya mji.
Aidha ametoa wito kwa wazazi kuendelea kuwasindikiza watoto wao shule ili kuhakikisha usalama wao.
Hiki ni tukio la pili ambapo Siku chache zimepita tangu mtoto Sporal Sambalya mwenye umri wa miaka 6 kujeruhiwa na fisi mjini Bariadi mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment