Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella amesema watu elfu tano kutoka maeneo mbalimbali nchini wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya Royal Tour jijini Arusha
Uzinduzi huo utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).
Mkuu huyo wa mkoa wa Arusha a,ewaomba wana Arusha na mikoa ya jirani, kushiriki kesho katika uzinduzi wa 'Royal Tour' lakini pia kushiriki kumlaki Rais Samia Suluhu Hassan ambaye atatua kesho saa 12 kamili
Aidha amesema vyombo vyote vya habari nchini vitaonyesha tukio hili mubashara na wananchi wote watapata nafasi ya kuona tukio hilo.
Kuhusu usalama wa jiji la Arusha amewatoa hofu wananchi na kuwataka kuwa na amani kwani vyombo vya usalama vipo imara.
"Jiji letu lipo salama, na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vipo timamu na tutahakikisha kuwa kila anayeingia na kutoka atakuwa salama yeye na mali zake"
Mbali na mgeni Rasmi Rais Samia Suluhu Hassan wageni wengine ni Makamu wa Rais, ugeni mkubwa kutoka Zanzibar, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Spika wa bunge la Tanzania, mawaziri mbalimbali , makatibu wakuu na viongozi wa vyama vya siasa
No comments:
Post a Comment