Sheikh waWilaya ya Kahama Omary Damka akiweka jiwe la msingi la Msikiti wa Ramadahan uliopo Igomelo Kahama
Sheikh wa Wilaya ya Kahama,Omari Damka,ametoa wito kwa Maimamu na Wallimu wa Madrasa sambamba na KAMATI za Misikiti kupanga mkakati wa kuwapatia Elimu ya dini vijana wanaosoma shule za Msingi na sekondari pasipo kuathiri masomo Yao.
Sheikh Damka alisema hayo wakati akiweka jiwe la Msingi la uendelezaji ujenzi msikiti mkubwa na Madrasa ya kisasa katika Masjid Ramadhani uliopo Igomelo,Kata ya Malunga Wilayani Kahama.
.
Alisema vijana wengi wa kiislamu hivi Sasa hawapati Elimu stahiki ya dini kutokana na wazazi pia Walezi kuweka kipaumbele Elimu dunia kwa vijana wao na kudharau Elimu ya dini Jambo ambalo limesababibisha mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa jamii.
Aliwapongeza kwa juhudi kubwa kwa kuendeleza Madrasa na harakati walizonazo za kielimu sambamba na kuibua wazo la kujenga msikiti mkubwa katika jengo ambalo awali lengo lilikuwa darasa japo lilitumika pia kwa masuala ya Ibada.
Aidha aliwaomba Waislamu kufanya Maendeleo katika sekta ya elimu ya dini ili vijana wajengeke katika maadili mema ili kuepukana na ombwe la mmomonyoko wa kimaadili unaoikumba jamii.
" Watu wanazingatiwa kwa tabia zao,kwa maadili yao mema,mtu anakuwa na heshima,mtu anapata hadhi,mtu anaheshimiwa,mtu anachaguliwa,mtu anapewa uongozi,"alisema Sheikh Damka.
Aliongeza, " sio Elimu tu itakayozingatiwa lakini kila atapopata kazi anaweza kufukuzwa,kwahiyo maadili mema na tabia nzuri Ni Jambo kubwa Sana katika maisha na si kujivunia nasabu.
Alisisitiza wazazi kuwalea watoto katika upendo na kuwafundisha adabu njema sambamba na Elimu ya dini na dunia ndipo watakapokuwa wamewapatia urithi mzuri kuliko kuwapatia Mali,mashaamba ama nyumba.
" Ile tabia ya kujinasibu Mimi mtoto wa Sheikh,Kiongozi ama mimi mtoto wa Fulani haisaidii,bali tabia na adabu njema ndio silaha katika maisha yao," alisema Sheikh wa wilaya.
Awali Sheikh Mwamfundo Juma,alisema wazazi sasa hivi wanahadaika na vitabu vya tafsiri vinavyouzwa madukani na kudai huwezi kuwa Elimu sahihi ya dini pasipo kusomeshwa.
Sheikh Mwamfundo alisema Elimu ya dini lazima uende kusoma kwa wanazuoni kwani hata Mtume Muhammad SAW alisomeshwa na Maalim wake Jibril,hivyo hakuna budi vijana kupita katika madarasa ya wanazuoni ili kuifahamu dini.
No comments:
Post a Comment