BUNGE LAAHIRISHWA KUPISHA EID EL-FITR - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 29 April 2022

BUNGE LAAHIRISHWA KUPISHA EID EL-FITR







Dodoma. Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson ameahirisha mkutano wa Bunge hadi Alhamisi ya Mei 5, 2022 saa tatu asubuhi.


Sababu ya kuahirishwa kwa siku zote imetajwa ni kutokana na kutokuwa na uhakika wa mwanadamo wa mwezi ambao utafanya uwepo wa sikukuu ya waumini wa dini ya Kiislamu inayoendana na mwandamo wa mwezi.


Spika amesema kulingana na tangazo la Mufti wa Tanzania kuwa huenda sikukuu ikawa kati ya jumatatu au siku ya jumaa, anaona busara kuahirisha Bunge hadi Alhamisi kwa kuwa hakutakuwa na siku ya kukutana tena.


“Waheshimiwa wabunge, kutokana na tangazo la Mufti ni ngumu kusema tunaweza kukutana tena na kupeana matangazo, kwa hiyo naona vema tuheshimu hilo na kwa hiyo naahirisha shughuli za bunge hadi alihamisi saa tatu asubuhi,” amesema Spika Dk Tulia.


Tangazo la Spika liliwaibua wabunge ambao walianza kushangilia kwa wingi wa makofi huku wengine wakisika kusema ‘udumu spika wetu’ kisha wakatawanyika.

chanzo:Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso