Matukio ya kikatili bado yanaendelea kuikumba Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi baada ya kutokea mauaji ya bibi kikongwe Marieta Thomas mwenye umri wa miaka 90 mkazi wa mtaa wa Mpanda hotel.
Bibi huyo ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasiofahamika.
Tukio
hilo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu ya Pasaka baada ya
majirani wa marehemu kugundua kuwa bibi kikongwe huyo ameuawa.
Akizungumza
kwa simu na mtandao huu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Katavi ACP Ally
Makame amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kuwa chanzo cha mauaji hayo
ni imani za kishirikina.
Aidha kamanda
Makame amesema licha ya kutokukamatwa kwa watu waliotekeleza mauaji hayo lakini
wanaodhaniwa ni wajukuu wa bibi huyo kutokana na kutokufika katika msiba huo.
No comments:
Post a Comment