BABU WA MIAKA 95 AUAWA KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA-NJOMBE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 23 April 2022

BABU WA MIAKA 95 AUAWA KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA-NJOMBE

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 95 wa Kijiji cha Lwanzali kilichopo Lupembe Halmashauri ya Wilaya ya Njombe amekutwa ameuawa ndani ya nyumba yake huku upelelezi wa awali ukionesha kuwa chanzo ni kutokana na Mzee huyo kutuhumiwa kufanya ushirikiana katika Familia yake.

RPC wa Njombe Hamis Issah amesema "Tumejaribu kwenda katika eneo lile na imebainika huyu Mzee walikuwa wanamtuhumu kuwa anafaya mambo kishirikina katika Familia yake”

Kamanda Issah amesema Polisi wanaendelea kuchunguza ili kubaini ni nani aliyehusika na mauaji hayo ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.


 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso