Polisi Mkoani Tanga wanamshikilia Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 kwa ajili ya uchunguzi akituhumiwa kumchezea Mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miezi 11 kwa kumpenyezea vidole sehemu zake za siri .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema Baba huyo wa kambo anaishi Mtaa wa mikocheni eneo la Amboni Jijini Tanga na kwamba tukio hilo lilitokea April 11,2022
"Mtoto alikuwa amebebwa mgongoni na Mama yake, yule Baba kwakuwa hiyo michezo hiyo ameizoea akampenyezea Mtoto kidole sehemu zake za siri na Mama alikuja kutoa taarifa Polisi"
Kamanda Jongo amesema Mama mzazi wa Mtoto ameeleza kwamba alibaini kuwepo kwa vitendo visivyo vya kawaida kwa Mtoto baada ya Mtoto kuwa na tabia ya kulia na kutoa harufu mbaya sehemu zake za siri.
"Baada ya uchunguzi wa daktari ikathibitika ni kweli sehemu za siri za Mtoto huyo zipo wazi , hajaingiliwa kimwili lakini sehemu zake za siri zipo wazi ina maana yule Mtoto alikuwa akichezewa kwa muda mrefu"
No comments:
Post a Comment