Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amesema kwamba mwananchi yeyote atakayefanikisha kutoa taarifa na kukamatwa kwa mtuhumiwa anayejihusisha wizi wa mifugo na uhalifu wa kutumia silaha atazawadiwa kiasi cha shilingi milioni moja.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro
IGP Sirro amesema hayo akiwa jijini Arusha wakati akizungumza na maofisa waandamizi wa wa jeshi hilo, ambapo pia akatumia nafasi hiyo kuwataka wafungwa wanaopata msamaha wa Rais kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi kwa kutojihusisha tena kwenye makosa ya uvunjifu wa sheria na kuwa kero kwa wananchi kwa kufanya vitendo vya kihalifu.
Katika hatua nyingine IGP Sirro, amewataka bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuvaa kofia ngumu huku.
No comments:
Post a Comment