Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Eliyasa Omari mwenye umri wa miaka 55 mkazi wa mkoani Tanga, amefariki dunia baada ya kukatwa mapanga na mwenzake kisa unga wa ugali na dagaa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Safia Jongo
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Safia Jongo, amethibitisha na kusema kwamba marehemu na mtuhumiwa wote ni vibbarua wa shamba la mkonge ambapo siku ya tukio wote walikuwa shambani na walivyorudi nyumbani mtuhumiwa alibaini kwamba simu, unga na dagaa wake wameibiwa.
"Kwahiyo akaanza kumtuhumu kibarua mwenzake ambaye wanaishi wote nyumba moja kwa takribani miaka miwili sasa, huyu akimtuhumu mwenzake kwamba kaiba na mwenzake akikataa kwamba hajaiba, ndipo ugomvi ulipoibuka," amesema Kamanda Jongo.
Kamanda Jongo amesema kuwa mtuhumiwa ni majeruhi na hali yake ni mbaya na amelazwa katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza.
Aidha Kamanda Jongo amewataka Watanzania pindi wanapoona watu wawili wanagombana wasiwaachie wamalizane kama wanaangalia sinema na badala yake wawaamulie kwani kuacha watu wapigane kunaweza kusababisha madhara makubwa.
No comments:
Post a Comment