Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe
imemuhukumu Fadhili Ngoho (25) mkazi wa Ulembwe, Wilaya ya Wanging'ombe mkoani
Njombe kwenda jela maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka Mtoto wa miaka
8.
Fadhili amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka Mtoto wa miaka 8 ambaye
ni Mtoto wake wa kambo aliyekuwa akisoma katika moja ya shule ya msingi iliyopo
katika kata ya Ulembwe.
Inaelezwa kuwa siku hiyo Mshtakiwa alimbaka Mtoto huyo na kumwambia asipige
kelele.
Hata hivyo Tarehe 23/2/2020 Mama wa Mtoto huyo alimuona Mwanae hatembei vizuri ndipo alipomuuliza ana tatizo gani na kisha Binti huyo akamwambia Mama yake kuwa Baba yake wa kambo alimbaka.
No comments:
Post a Comment