TANZANIA YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU VITA YA UKRAINE NA URUSI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 24 March 2022

TANZANIA YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU VITA YA UKRAINE NA URUSI



Siku moja baada ya Ujumbe wa mabalozi wa nchi za Ulaya nchini Tanzania kuitaka Tanzania na nchi nyingine za Afrika kupaza sauti kukemea uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, nchi hiyo imetoa msimamo wake leo na kusema yenyewe haifungamani na upande wowote.


Msimamo huo unapigiwa mstari na uamuzi wa taifa hilo la Afrika Mashari la kutokupigia kura azimio la baraza Kuu la Umoja huo, UNGA kupitisha lililopitishwa mapema mwezi huu, kuitaka Urusi kusimamisha mara moja mashambulizi yake dhidi ya Ukraine na kuyaondoa majeshi yake katika nchi hiyo.


Waziri wa Masuala ya kigeni wa nchi hiyo, Liberata Mulamula amesema kwa miaka mingi sasa Tanzania inaamini katika kutafuta muafaka na marudhiano kwa kutumia njia ya diplomasia ili kumaliza migogoro.


Kutokana na muafaka na maridhiano kutopatikana katika mzozo wa Urusi na Ukraine, Waziri Mulamula anasema: “ndio maana katika kupiga tukaamua kutofungamana na upande wowote, lakini ilikuwa sio kutofungamana na pande zote mbili lakini ni kutoa ujumbekuonyesha kwamba sisi msimamo wetu na sera yetu na msingi wetu wa sera ya mambo ya nje ni kutokufungamana na pande zozote hasa katika hali kama hii”, alisema Mulamula.


Tanzania ilikua miongoni mwa mataifa 35 wanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo hayakupiga kura kuunga wala kukataa azimio hilo lililoungwa mkono na mataifa 141, huku mataifa matano ya Urusi, Belarus, Syria, Korea Kaskazini na Eritrea, yakipinga azimio hilo.


Hapo jana ujumbe wa Mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya nchini Tanzania pamoja na kuzitaka nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kupaza sauti zao kulaani uvamizi huo wa Urusi, waliitaka pia Urusi kumaliza mzozo wake na Ukraine bila kupigana vita.

Chanzo: BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso