JAMII YAASWA KUFUNDISHA VIJANA TABIA NJEMA KUEPUKA VITENDO VYA KIKATIRI. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 28 March 2022

JAMII YAASWA KUFUNDISHA VIJANA TABIA NJEMA KUEPUKA VITENDO VYA KIKATIRI.




Wazazi na Walezi wameaswa kuhakikisha wanajikita katika kufundisha vijana tabia njema kutokana na kipindi hiki cha utandawazi jamii kukabiliwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili unaosababisha kufanyiana vitendo vya kikatiri ikiwemo kubakana na kuuana.

Kauli hiyo ilitolewa na Sheikh wa Wilaya ya Kahama,Omari Damka,wakati akimuwakilisha Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga,Habibu Makusanya,kuweka Jiwe la Msingi katika Msikiti wa Ramadhani uliopo Igomelo wilayani Kahama.
 
Sheikh Damka alisema ni budi wazazi kushikamana na viongozi wa dini sambamba na walimu wa kada mbalimbali katika kutoa elimu huku wakiongoza ufundishaji wa maadili mema kwa vijana ili kuinusuru jamii na matukio ya ukatiri mbalimbali.
 
Alisema kukithiri kwa tabia ovu,ikiwemo ukatiri wa ubakaji na mauaji mbalimbali yakiwemo ya vikongwe ni kutokana na jamii kutoweka umuhimu katika elimu ya dini huku malezi yao nyumbani yakitawaliwa na mabadiriko ya utandawazi.

Sheikh Damka alisema ili kukabiliana na mabadiriko hayo yanayosababisha na utandawazi ni jukumu la wazazi na walezi kufundisha vijana wao maadili mema.

Alisema vijana wengi watendelea kusononeka kutopata ajira licha ya kuwa na elimu kubwa pasipo kufahamu kinachowaangusha ni kutokuwa na maadili mema ambayo huwa chachu ya kukubalika katika jamii.

Aliwakumbusha wazazi ni budi kufanya maendeleo katika familia zao huku suala la maadili mema wakilipa kipaumbele ili kuandaa taifa lenye misingi bora ya uzalendo utakaosababisha maendeleo stahiki ya taifa.
 
Aidha kwa upande wake Sheikh Mamfundo Juma,alisisitiza umuhimu wa vijana kupata elimu sahihi kupitia eneo sahihi na si kujiona wasomi kwa kupata elimu kupitia vitabu wanavyonunua dukani na kuvisoma pasipo kupata ufafanuzi wa kielimu kutoka kwa wajuzi wa elimu hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu ( BAKWATA ) wilaya ya Kahama,Haji Nasser,aliisisitizia jamii kuwa wepesi wa kukabidhi maeneo ya ardhi katika Taasisi za Kielimu.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso