Ushirikiano wa Jeshi la Polisi na wananchi wa Halmashauri ya Msalala,wilaya ya Kahama,mkoani Shinyanga,umefanikisha kupatikana kwa mtoto mchanga aliyekuwa ameibiwa wodini katika Kituo cha Afya Lunguya,Halmashauri ya Msalala,kitendo kikichopongezwa na Serikali wilaya ya Kahama.
Akitoa pongezi hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Kahama,Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Festo Kiswaga,alisema ushirikiano ulioneshwa na jeshi la Polisi na wananchi ni la kupongezwa,kutokana na kufanikisha kupatikana kwa mtoto huyo kwa wakati na kiwa na afyua njema.
Mkuu huyo wa wilaya alisema Jeshi hilo la Polisi wilaya ya Kipolisi Msalala,linapaswa kushukuriwa kwa kutekeleza majukumu yao,ambayo ana hakika haikuwa kazi rahisi kufanikisha kupatikana kwa mtoto huyo.
“ Pia hapana budi kuwashukuru wananchi waliojitokeza kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa muhimu zilizofanikisha kupatikana kwa mtioto huyo,jambo ambalo ni lakujivunia kuona mashirikiano hayo,”alisema Kiswaga.
Alisema ni vyema wananchi wakaendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi,kama amabvyo walivyomudu kufichua ouvu uliotokea Kituo cha afya Lunguya mnamo Februari 2,mwaka huu,ushirikiano utakaoliwezesha jeshi la polisi kufanya kazi yake kwa ufanisi na kuifanya wilaya ya Kahama kuwa katika hali ya amani na utulivu.
Kiswaga alisema tukio hilo la Kituo cha Afya Lunguya,lilitokea majira ya saa 05:30,kwa mtoto wa kiume wa siku moja tangu kuzaliwa kuibiwa wodini akiwa kitandani,kitendo ambacho hakikuwa cha kawaida na kilenga kuchafua taswira ya Kituo hicho cha Afya na wilaya ya Kahama.
"Mnamo tarehe 30/01/2022 majira ya saa 10:00 Mama wa mtoto huyo aitwaye Bertha Augustino (20) mkazi wa Ntambarare kata ya Segese akitokea Zahanati ya Segese na kupelekwa Kituo cha Afya Lunguya kwa Rufaa, alifanyiwa upasuaji na kujifungua mtoto huyo wa kiume na kubakia wodini kwa uangalizi zaidi wa kitabibu",amesema Kiswaga.
"Mama huyo akiwa pale wodini kabla na baada ya kujifungua alionekana akipewa huduma zingine na mwanamke mmoja mnene, mweusi, mwenye macho ya makengeza ambaye wauguzi walipotaka kujua mwanamke huyo ana uhusiano gani na mzazi, Mama na Baba wa mtoto walieleza kuwa hawamfahamu.Ndipo ghafla siku hiyo ya tarehe 1/2/2022 majira ya saa 05:30 ilikuja kubainika mtoto huyo ameibwa na mwanamke aliyekuwa akimhudumia mama wa mtoto huyo naye ametoweka",ameeleza Kiswaga.
Amesema kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi lilianza upelelezi wa tukio hilo mara moja ambako waliweza kufika Geita, Sengerema, Kasulu, Masumbwe na Kahama katika ufuatiliaji wao.
"Mnamo tarehe 16/2/2022 majira ya saa 23:30 usiku huko kijiji cha Kakumbi Kata ya Lubunga Wilaya ya Mbogwe Mkoa wa Geita askari wa Polisi Msalala walifanikiwa kumkamata mwanamke mmoja aitwaye Rehema Said (47) mkazi wa Lubunga akiwa amelala ndani mwake na mtoto mchanga wa kiume",amesema.
"Ndugu wanahabari, baada ya kufikishwa Polisi Bugarama Wilaya ya Kipolisi Msalala, wazazi wa mtoto waliweza kumtambua mtoto wao na pia mwanamke huyo alitambuliwa kuwa ndiye aliyekuwa akimsaidia mama wa mtoto na kumuiba pale Kituo cha Afya Lunguya",ameongeza Kiswaga.
Amesema Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara tu upelelezi wa kesi hii utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment