Baadha ya mambo ni kama vile, viwango vya chini vya mishahara, licha ya kwamba taifa hilo linapitia hali ngumu ya kiuchumi. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wiki iliyopita Tunisia ilirejea kwenye mashauriano na shirika la kimataifa la fedha kuhusiana na mkopo uliosimamishwa kutokana na Tunis kuchukua hatua za kuwa na uchumi huru.
Mashirika ya misaada ya kimataifa pia yamesema kwamba kuna umuhimu wa Tunisia wa kufanya marekebisho ili kukabiliana na ufisadi na matumizi mabaya ya fedha, ikiwa na maana kwamba huenda serikali ikahitaji uungaji mkono wa UGTT ambao unawakilisha takriban wafanyakazi milioni moja, wakati likiwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa wa kutosha kuishawishi IMF.
Jumatatu waziri mkuu Najla Bouden pamoja na serikali yake wamefanya kikao na kiongozi wa muungano wa UGTT Noureddine Taboubi, pamoja na maafisa wengine kwa lengo la kuzungumzia hali iliyoko ya kiuchumi. Taboubi amesema kwamba mkutano huo wa kwanza na serikali ulienda vyema na kwamba mambo yaliyokubaliwa yatatangazwa baadaye.
Mwaka uliopita serikali ilitangaza pendekezo la kuongeza mishahara ya takriban wafanyakazi 700,000 kwenye sekta ya umma, pamoja na kuongeza viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wote nchini.ser
No comments:
Post a Comment