CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Barcelona wanafikiria uhamisho wa mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling,26. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Barcelona wamebaki kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa zamani wa Uhispania Xavi, 41, kuhusu kuchukua nafasi ya kocha Ronald Koeman. (90min)
Everton ilijaribu kumsajili Donny van de Beek, 24, kwa mkopo kutoka Manchester United na ingependa kumchukua kiungo huyo wa kati wa Uholanzi mwezi Januari. (NOS via Mail)
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Manchester United inafikiria kumpata kiungo wa kati wa AC Milan Franck Kessie,24, kama mbadala wa Paul Pogba. (Calcio Mercato - in Italian)
Inter Milan wako tayari kurejesha nia yao ya kumpata beki wa pembeni wa Chelsea, Mhispania Marcos Alonso,30. (Tutto Mercato - in Italian)
Manchester City wanashinda mbio za kumnasa mlinzi wa Villarreal na Uhispania,24, Pau Torres. (Metro)
Tottenham inaweza kumtimua kocha Nuno Espirito Santo bila kulipa fidia yoyote ikiwa hatawaongoza kufikia nafasi sita za juu kwenye ligi Primia. (Athletic - subscription required)
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Kiungo wa kati wa Pogon Szczecin, Kacper Kozlowski, 17, ambaye amekuwa akifuatiliwa na Liverpool, AC Milan na RB Leipzig, amesema havutiwi na ''majina makubwa''. (Sport Interia - in Polish)
Kocha wa Everton Duncan Ferguson alikwenda kumfuatilia mlinzi wa kati wa Stoke City, Harry Souttar,22, wakati the Toffees wakipanga uwezekano wa kuondoka kwa Yerry Mina. (Sun)
Monaco imetangaza dau la pauni milioni 34 kwa kiungo wa kati Aurelien Tchouameni, 21, kwa Juventus na Chelsea. (Calciomercato - in Italian)
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Manchester City wanamfuatilia kiungo wa kati wa Uhispania Nico Gonzalez anayekipiga Barcelona, ambaye hajapewa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza . (Fichajes - in Spanish)
Wakati huohuo, mlinzi Sergi Roberto ni mchezaji mwingine wa Barcelona anayetolewa macho na Manchester City, wakati mkataba wa mchezaji huyo huko Nou Camp ukitarajiwa kumalizika majira ya joto yajayo. Calciomercato - in Italian)
Claudio Ranieri amekubali kuwa kocha mkuu mpya wa Watford baada ya kuondoka kwa Xisco Munoz siku ya Jumapili, huku Muitaliano huyo, 69 akitarajiwa kuweka saini Jumatatu. (Sky Sports)
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Mlinzi kinda wa Kijerumani anayecheza katika klabu ya Borussia Monchengladbach Luca Netz anadai alikataa uhamisho aliosema ''hauna maana'' kwenda Manchester City miaka mitatu iliyopita, mchezaji huyo mwenye miaka 18 anasema atawakatalia kwa mara nyingine tena. (Sun)
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Alexis Sanchez hajui mustakabali wake Inter Milan baada ya mchezaji huyo mwenye miaka 32-kuchapisha kisha kufuta ujumbe uliokuwa ukikosoa kitendo cha kukosa muda wa kucheza uwanjani. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure, 38, ametoa ofa kwa Barcelona wakati huu wakiwa katika changamoto, lakini haijulikani kama raia huyo wa Ivory coast anataka kucheza au kufundisha. (Sun)
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Atletico Madrid nayo imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnasa mshambuliaji Timo Werner, 25 anayekipiga Chelsea. (Transfer Market Web)
Mmiliki Mike Ashley anajua njia pekee ya kumbadili kocha mkuu wa Newcastle ni kulipa karibu kila kandarasi ya Steve Bruce ambayo alikubali mnamo Julai 2019.(Chronicle Live)
Mshambuliaji wa Kiholanzi anayecheza Bayern Munich Joshua Zirkzee, 20, anasema alikataa nafasi ya kujiunga na Everton mwaka 2017. (Het Nieuwsblad via Liverpool Echo)
No comments:
Post a Comment