Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) nchini Tanzania kimetoa taarifa kwa umma kujibu tuhuma dhidi ya mwanataaluma wa chuo hicho.
Taarifa hiyo inasema "chuo kilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tuhuma dhidi ya mtumishi wake ndugu Petro Bazil Mswahili ambaye ni Mwanataaluma juu ya kujihusisha na rushwa ya ngono kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma".
Chuo hicho kimesema, mwalimu huyo amesimamishwa majukumu yake yote kuanzia Oktoba 25 mwaka huu hadi uchunguzi utakapokamilika.
Tayari , Chuo kimeanzisha mchakato wa hatua za kinidhamu na maadili kulingana na sheria na kanuni za utumishi wa umma.
Aidha, Chuo kinapenda kuutaarifu Umma kuwa kitendo hiki hakivumiliki wala kukubalika na kwamba wakati wote Chuo kitaendelea kusimamia nidhamu na maadili kwa watumishi wake wote.
Pia, Chuo kitaendelea kuchukua hatua kali kwa mtumishi yeyote atakayebainika kujihusisha na makosa ya kinidhamu. Chuo kimesikitishwa sana kwa usumbufu uliojitokeza.
No comments:
Post a Comment