Baadhi ya wakazi wamekwama katika maeneo ya chini ya nyumba zao yaliyofurika maji pamoja na ndani ya magari yao
Rais wa Marekani Joe Biden anasema "uwekezaji wa kihistoria " unahitajika kukabiliana na mzozo wa hali ya hewa, huku maeneo ya kaskazini-magharibi mwa nchi yakikabiliwa na mafuriko pamoja na vimbunga ambavyo vimewauwa watu wapatao 41.
Marekani inakabiliwa na uharibifu unaotokana na hali ya hewa kote nchini na kushughulikia uharibifu huo ni "suala la maisha na kifo ", alisema rais.
Majiji ya New York City na New Jersey yalishuhudia mvua kubwa ambayo haikutarajiwa.
Baadhi ya wakazi wamekwama katika maeneo ya chini ya nyumba zao yaliofurika maji pamoja na ndani ya magari yao.
No comments:
Post a Comment