Jeshi la Polisi mkoani Morogoro,linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuchoma moto mali za Serikali zikiwemo;gari aina ya Land Cruiser,Pikipiki tatu,Kompyuta mpakato tatu na kifaa cha kupimia mipaka ya ardhi.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro,Fortunatus
Musilim,alisema tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Melela kata ya Chita
Wilaya ya Kilombero.
Kamanda
Muslim,alidai watuhumiwa hao kutenda kosa hilo baada ya maafisa wa Ardhi kufika
katika shamba linalomilikiwa na marehemu Daud Balali ambaye alikuwa Gavana wa
Banki kuu ya Tanzania,kwa lengo la kupima mipaka ya shamba.
Aidh Musilim ameongeza kuwa katika
tukio hilo dereva aliyefahamika kwa jina la Damas Sanga (51 ) alijeruhiwa baada
ya wananchi hao kumkukuta kwenye gari na kuanza kumshambulia sehemu mbalimbali
za mwili wake.
Kwa upande wake kamishina msaidizi
wa Ardhi mkoa wa Morogoro,Frank Minzikuntwe,alisema vurugu hizo zimetokea baada
ya maamuzi ya serikali ya kulipima shamba hilo ili liweze kupangwa upya
matumizi yake baada ya kutelekezwa kwa muda mrefu huku wananchi
wanalolizunguuka wakikosa maeneo ya kulima.
No comments:
Post a Comment