MESSI AACHANA RASMI NA BARCELONA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 6 August 2021

MESSI AACHANA RASMI NA BARCELONA







Barcelona ikijaribu kumbakiza Lionel Messi, inaweza kuiweka klabu hiyo katika hatari kwa miaka 50 ijayo, hiyo ni kwa mujibu wa rais wa klabu hiyo, Joan Laporta.

Messi, 34, anaondoka Barcelona kwa sababu klabu hiyo imeshindwa kumpa mkataba mpya kutokana na kubanwa na kanuni za La Liga kuhusu mishahara ya wachezaji.


Inaelezwa kuwa , kulikuwa na kampuni binafsi iliyotaka kuwekeza La Liga, hatua ambayo ingewezesha usajili wa Messi, lakini wakati huo huo, ingemaanisha Barca iachane na haki za matangazo ya Televisheni.

"Siwezi kufanya uamuzi ambao utaiathiri klabu kwa miaka 50 ijayo," alisema Laporta.

"Klabu hiii ina miaka zaidi ya 100 na iko juu ya kila kitu na kila mtu akiwemo mchezaji bra duniani. Siku zote tutamshukuru kwa kila kitu alichotufanyia.

"Ili kuwa kukidhi matakwa, tunahitaji kufanya tulilofanya, au kuiweka klabu katika wakati mgumu, Hatukuweza kuendelea na hilo, na tulipaswa kufanya uamuzi, tuliofanya."

Messi, mfungaji bora wa Barcelona wa muda wote, alikubali mkataba wa miaka 5 uliopunguzwa mshahara wake- lakini ili kufanikisha usajili wake, Klabu hiyo ilipaswa kuendelea kupunguza kiwango cha matumizi ya mishahara , kitu ambacho imeshindwa.

"Leo alitaka kubaki, kwa hivyo hajafurahia hili," alisema Laporta. "Sote tulitaka abakie. Kwa Messi anatakiwa akubaliane na hali halisi. Ndio ukweli ambao hauwezi kubadilika, na anafahamu, namtakia mema popote atakapokwenda."

Laporta aliongeza kuwa hakutaka kutoa matumaini ambayo hayapo kwamba angeweza kumbakiza Messi. "Mjadala umefungwa," alisema.(BBC SPORT)

Tangazo la Barcelona kwamba mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, hatabakia kwenye klabu hiyo ''limefungua mlango wa uhamisho wa kushtua " katika Manchester City. (Manchester Evening News)

Uwepo wa Messi unaweza kuathiri uwezekano wowote wa uhamisho ambao Man City walikuwa wanaupanga kwa ajili ya mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27. (Express)

Paris St-Germain wamekuwa wakihusishwa moja kwa moja na Messi, lakini jiji kuu la Ufaransa linaonekana tu kama moja ya maeneo ambayo anaweza kwenda Muargentina huyo anayesakwa na klabu nyingi . (Le Parisien - in French)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso