UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Simba wapo tayari na wanaamini kwamba watapata matokeo chanya.
Ikiwa inanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi,ipo nafasi ya pili na pointi zake ni 67 inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 73.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kikosi kipo imara na wanaamini kwamba watapata matokeo ila jambo la msingi ni kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti.
"Mechi itakuwa ngumu na ushindani ni mkubwa ila tupo tayari na tunachohitaji ni kupata ushindi kwani kila kitu kinawezekana.
"Jambo la msingi ni kuona kwamba lazima wapinzani wetu wanakuja katika muda uliopangwa, sisi tupo tayari," amesema.
Mchezo wa kwanza ulitarajiwa kuchezwa Mei 8 uliyeyuka baada ya kutokea mabadiliko ghafla ya muda ambapo awali ilipangwa kuchezwa saa 11:00 jioni taarifa ikatolewa kwamba utachezwa saa 1:00 usiku.
Kutokana na jambo hilo, Yanga iligomea mabadiliko hayo kwa kueleza
No comments:
Post a Comment