Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameongeza wiki mbili nyingine za “lockdown” kama njia mojawapo ya kupunguza maambukizi ya Covid- 19 nchini humo.
Hatua hiyo imekuja kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini Afrika ya Kusini.
Ramaphosa alisema kuwa shule zitaendelea kufungwa na kuendelea kuzuia mikusanyiko katika sehemu mbalimbali ikiwemo sehemu za starehe.
Huku sehemu za mazoezi na migahawa katika sehemu mbalimbali ya miji ikiruhusiwa kufunguliwa kwa sharti la wateja wao kukaa mbalimbali. “Serikali itaongeza fedha katika mfuko wa Covid ili kufidia biashara zilizoathiriwa,” Rais Ramaphosa
Afrika Kusini imeripoti maambukizi mapya 16,302 siku ya Jumapili yakileta jumla ya idadi ya maambukizi kuwa 2,195,599.
Jana watu 151 walifariki kwa sababu ya Covid na kusababisha idadi ya vifo kufikia 64,289
No comments:
Post a Comment